Siku ya Jumatatu,mkaazi mmoja wa mji wa Kazkazini Mashariki wa Gwoza amesema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao, wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka ndani ya nyumba kubwa karibu na kwake.
Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Amnesty International inasema kuwa takriban wanawake 2000 na wasichana wametekwanyara na Boko Haram tangu mwanzo wa mwaka uliopita.
Rais Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita watapatikana wakiwa salama.
Msemaji wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls ,Aisha Yesufu, aliiambia BBC kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa.
Lakini rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzai kinachosimamia jimbo na Borno kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.
No comments:
Post a Comment