Tevez aliwakusanya ndugu, jamaa na marafiki na kufanya dua hiyo, Ijumaa
iliyopita nyumbani kwao Msamvu, Madawa jirani na Shule ya Msingi Msamvu
‘A’ ambapo alifanya kisomo hicho kilichoambatana na dua na chakula.
“Mungu amemnusuru na balaa lile, amemkingia hivyo ameona ni vyema aandae
dua ya kumshukuru,” alisikika mmoja wa waalikwa.Baadhi ya mashehe na
waumini wengine wa Kiislamu waliohudhuria dua hiyo walimpongeza Tevez
kwa kitendo hicho cha kumkumbuka Mungu na kumshukuru kwa kumlinda na
majanga yaliyomkuta.
“Hili ni jambo jema sana alilofanya Tevez ambapo tunaelekezwa na mitume
wetu kwamba tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema mmoja wa waumini
wa dini ya Kiislamu.Kwa upande wake Tevez alisema amamshukuru Mungu
kwani amempigania sana uhai wake.
“Lilikuwa ni tukio kubwa kwangu, sikutegemea kama ningenusurika, Mungu
amenipigania sana nimeona bora nijumuike na ndugu, jamaa na marafiki
kumshukuru Mungu,” alisikika Tevez.Januari mwaka huu, Tevez alitekwa na
watu wasiojulikana katika mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambapo
mwenyewe alibainisha kuwa mwenyeji wake mjini humo alivujisha habari
kuwa ana fedha ndipo akavamiwa, akateswa na kuporwa fedha na simu zake
mbili
Tevez aliwafungulia mashtaka vijana waliohusika na tukio hilo ambapo kesi inaendelea kuunguruma nchini humo.

No comments:
Post a Comment