Rais mteule wa Nigeria Jenerali Muhhamadu Buhari akishangilia baada ya APC kushinda majimbo makuu ya Lagos kaduna na Katsina katika uchaguzi wa Mgavana na Wabunge uliofanyika jumamosi na jumapili.
Mfanyakazi wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria INEC akiwaelekeza jambo wapiga kura.
Raia wa Nigeria walivyokuwa wakipiga kura kuwachagua Magavana na Wabunge.
Chama cha The All Progressives Congress (APC) kilichoshinda katika Uchaguzi wa Rais kupitia mgombea wake Bw. Mahammadu Buhari nchini wiki chache zilizopita, kimeshinda majimbo makuu ya Lagos Kaduna na Katsina katika uchaguzi mkuu wa magavana na wabunge nchini humo.
Ushindi huu unaiongezea nguvu serikali mpya haswa baada ya kutwaa ushindi mkubwa dhidi ya Rais Goodluck Jonathan. Matokeo kamili ya kura za majimbo 39 na magavana 29 unatarajiwa kutolewa baadaye.
Magavana 29 kati ya wale waliochaguliwa wanaonekana kukubalika zaidi na licha na ushawishi mkubwa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kiuchumi. Uchaguzi huu wa majimbo umeendeleza dhana ya kuwa APC itazoa maeneo mengi ya uwakilishi kufuatia ushindi wa kihistoria wa jenerali mstaafu Muhammadu Buhari.
Siku ya jumapili, tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria (INEC) ilitangaza rasmi kuwa chama cha Jenerali mtaafu Buhari APC ilikuwa imetwaa jimbo la Lagos mbali na kushinda ugavana wa majimbo ya Kaduna na Katsina majimbo ambayo yaliongozwa na kudhaniwa kuwa ni ngome ya Chama cha PDP.
Hata hivyo Chama cha PDP kilishinda jimbo la Rivers linaloongoza kwa kuwa na uzalishaji mkubwa wa mafuta nchini humo. Kwa wadadisi wengi utawala wa Jenerali mstaafu Buhari utakuwa utawala wa kwanza kutawala nchi na vilevile mji mkuu wa kiuchumi nchini humo wa Lagos tangu kumalizika kwa utawala wa kiimla mwaka wa 1999.
Vilevile hii ndio itakayokuwa mara ya kwanza kwa chama ambacho sio PDP kuwahi kuiongoza majimbo ya Kaskazini mwa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment