| Akilazimishwa kula maindi hayo. |
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, baada ya kumnasa kijana huyo akiiba mahindi aliyoyajaza kwenye gunia, wamiliki wa shamba hilo walimuamuru kukaa chini na kuyala yakiwa mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo alikubaliana nacho.
Ilielezwa kwamba, katika hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa wala kuonesha kutetereka kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha na kuambiwa aondoke.Katika habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa Harakati, kijana huyo alionekana kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri wala kuongea kwa maana ya kuwa ni ‘bubu’.
Hata hivyo, kijana huyo hakujulikana alitokea wapi kwani mbali na madai ya wizi na ububu pia hakuonekana mwenye ufahamu mzuri kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa.
No comments:
Post a Comment