Viongozi wawili wa dini nchini
Kenya wameiambia BBC kwamba wamepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa
wapiganaji wa kundi la Alshabaab wiki tatu tu baada ya shambulizi katika
chuo kikuu cha Garissa.
baadhi ya jamii na familia zilizoathiriwa na shambulizi la Garissa
Viongozi hao pia kutoka Garissa wamesema baadhi ya viongozi wa dini wamepokea vitisho katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.
Wana wasiwasi kwamba serikali inawashirikisha katika vita dhidi ya wapiganaji wa Al shabaab bila kuwahakikishia usalama wao.
Viongozi
hao walikuwa wakizungumza baada ya kushiriki katika mkutano wa vita
dhidi ya itikadi kali pamoja na viongozi wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment