| Mji huo wa Kobane uliharibiwa pakubwa baada ya vita vilivyoongozwa na Wakurdi kwa muungano na Marekani |
Jaribio lla kuteka miji ya Kobane na Hassakeh ni ilani kwa ulimwengu kuwa huenda wapiganaji hao wamepata nguvu mpya.
Kundili la wachunguzi wa Human Rights limesema vita hivyo vilianza baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwa gari kulipuka katika eneo la kuvukia.
Wapiganaji wa Kikurdi wanaoungwa mkono na jeshi la Marekani linaloongoza mashambulizi ya angani walikuwa wameteka mji huo wa Kobane katika tukio lililoonyesha ushindi mkubwa dhidi ya IS.
Kuna taarifa kuwa wapiganaji wa Islamic State waliingia mji wa kaskazini Hasake na kuteka maeneo mawili yaliokuwa yakithibitiwa na serikali.
No comments:
Post a Comment