Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
ameitaka timu yake kutafuta ushindi wa mapema katika pambano la mwishoni
mwa wiki hii Jumamosi dhidi ya Reading. Kocha huyo raia wa Ufaransa
amesema kuwa vijana wake wanapaswa kuanza kwa kasi na nguvu katika
mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Wembley kama kweli wanahitaji
kutetea taji lao.
Mechi hiyo itakuwa ni nusu fainali ya kumi kwa mzee Wenger ,huku akidai kwamba Arsenal inajiamini hasa kutokana na kushinda mechi nane mfululizo. Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili ambapo Aston Villa itawakaribisha Liverpool.
No comments:
Post a Comment