Jarida la Starsport limebainisha
kuwa Liverpool na Arsenal zinapanga makubaliano ambayo yatazifanya timu
hizo mbili kubadilishana wachezaji wawili wa taifa la Uingereza.
Walcott angejiunga na Liverpool msimu uliopita iwapo Luis Suarez angejiunga na Arsenal.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa tayari kumuachilia Walcott kujiunga na Liverpool lakini Suarez akabadili nia na kujiunga na Barcelona.
Sasa mpango kama huo umeanza kuandaliwa huku Sterling mwenye umri wa miaka 20 akipendelea kujiunga na Arsenal naye Walcott akikosa fursa ya kuanzishwa katika kilabu ya Arsenal.
No comments:
Post a Comment