Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa
Tanzania Peter Kuga Mziray amesema mwenendo wa Tume ya Uchaguzi
kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura hauridhishi na unatoa
viashiaria vya uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa
Tanzania Peter Kuga Mziray amesema mwenendo wa Tume ya Uchaguzi
kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura hauridhishi na unatoa
viashiaria vya uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba
na kuwaongezea muda viongozi waliopo akiwemo Rais Kikwete.
Mziray amesema kuwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) katika suala la uboreshaji wa daftari la wapiga kura na
upigaji kura ya maoni imeshindwa kufanya kazi yake na hivyo inatakiwa
kuachia ngazi mara moja.
Mziray ambaye pia ni mwenyekiti wa chama
cha APPT-Maendeleo amesema hayo jana wakati akiwa katika kipindi cha
HOT MIX cha EATV ambapo amedai kuwa tume hiyo ilijua tangu zamani kuwa
kufikia mwaka huu daftari lilipaswa kuwa limeboreshwa lakini lakini cha
kushangaza hadi sasa kazi ya uboreshaji haina matumaini yoyote kama
itamalizika kwa wakati.
“Kwa mujibu wa ratiba ya Tume, mwezi
wa nane mwaka huu ni kipindi cha wagombea kuanza kuchua fomu za urais,
sasa itamaliza kazi hiyo lini? Inasema mwezi wa saba lakini hiyo
haiwezekani, hii inaweza kuwa ni janja ya kuwaongezea viongozi waliopo
muda kwa njia ya kuahirisha uchaguzi” amesema Peter Mziray.
Amesema Baraza la Vyama vya Siasa na
chama chake cha APPT – Maendeleo haviko tayari kuona Rais Kikwete
akiongezewa muda, jambo la msingi ni viongozi wote wa tume kujiuzulu
nafasi zao kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi yao kwa wakati.
Kuhusu hatma ya katiba mpya, amesema
kuwa ni vyema serikali ifanyie marekebisho katiba iliyopo ya mwaka 1977
katika maeneo ambayo Kituo cha Demokrasia na Rais Kikwete walikubaliana
ambayo ni pamoja na kuwepo tume huru ya Uchaguzi, Matokeo ya uchaguzi wa
Rais kupingwa mahakamani na kuwepo kwa mgombea huru .

No comments:
Post a Comment