Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo akijipiga picha.
Obasanjo amekuwa akimwagiwa sifa kibao kutokana na kwamba yeye ndiye aliyeruhusu kuingia kwa simu za mkononi wakati akiwa madarakani, jambo ambalo limerahisisha shughuli za watu wengi nchini humo kutokana na teknolojia yake.
Pamoja na kwamba umri wake ni mkubwa sasa, bado kiongozi huyo wa zamani ana muda wa kupumzika na kutaniana na marafiki zake wakati hana mzigo tena wa kuisimamia nchi yake mbali na kutoa ushauri tu anapotakiwa.
No comments:
Post a Comment