Mtanzania aliyekamatwa Kenya akishukiwa kuhusika na shambulio la
kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliyopita lililosababisha
vifo vya watu takribani 150 na wengine wengi kuachwa majeruhi, Rashid
Charles Mberesero mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi wa kidato cha
tano katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma, lakini uongozi wa
shule hiyo umesema kuwa, Rashid alitoweka shuleni hapo tangu Desemba
mwaka jana.
 |
| Mtanzania aliyekamatwa Kenya akishukiwa kuhusika na shambulio la
kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliyopita Rashid Charles
Mberesero. |
Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kwamba mwanafunzi huyo
anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu
katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.
Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani
Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya
watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi.
CHANZO: ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment