Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye jina
lake linatajwa kutaka kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, anaelezwa kutamani kuingia katika
hatua za mwisho za kinyang’anyiro hicho na Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa.
Vyanzo
vya habari ndani CCM vinasema kwamba Membe amekua akionyesha kutamani
kuingia katika hatua ya 'tatu bora' pamoja na Lowassa ili aonyeshe uwezo
wake ndani ya chama hicho, tofauti na wapinzani wake wanaodai hana
nguvu kisiasa na hawezi kushindana na Lowassa ndani ya chama.
"Membe
anatamani sana kama akigombea aingie na Lowassa katika hatua ya mwisho
maana anatamani aonyeshe uwezo wake, kama alivyowaonyesha katika
uchaguzi wa kuingia NEC (Halmashauri Kuu ya CCM) mwaka 2012, ambao
walimpiga vita na kutumia fedha nyingi lakini akapata kura za kutosha
bila kampeni ya nguvu na kuwatia aibu," anasema mtoa habari huyo ndani
ya CCM.
Katika
uchaguzi huo wa mwaka 2012 ambao Lowassa hakugombea katika ngazi ya
Taifa na badala yake aligombea kupitia Wilaya ya Monduli, Membe alipata
kura 1,455 ikiwa ni asilimia 74 ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja
na kupigwa vita na wanasiasa ili asipite na kuingia NEC.

No comments:
Post a Comment