HATUA
ya mawakili wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,
kutengeneza ubishi wa kisheria katika agizo la Polisi la kuwasilisha
nyaraka za mali za Askofu huyo, imeelezwa kuwa ni ukaidi ambao
hautamsaidia kisheria.
Badala
yake, kwa hatua hiyo ya mawakili hao, Jeshi la Polisi limewekewa
mazingira mazuri ya kuchukua hatua ya pili ya matumizi ya nguvu katika
kutekeleza agizo lao, baada ya hatua ya hiyari kushindikana.
Wakizungumza
na gazeti hili jana, wanasheria mbalimbali walishangazwa na ubishi wa
juzi, uliotokana na barua ya mawakili wa Askofu Gwajima kwenda kwa Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Katika
barua hiyo, mawakili hao walitaka Polisi itoe agizo la maandishi la
kuwasilisha nyaraka hizo, litakaloeleza vifungu vya sheria vinavyomtaka
mteja wao kuwasilisha nyaraka hizo.
Ukaidi wa Gwajima
Barua
hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala, iliwasilishwa juzi mchana
katika jeshi hilo ikiwa ni siku moja baada ya Askofu Gwajima kutakiwa
kuwasilisha nyaraka 10 zinazohusu umiliki wa mali zake, Aprili 16 mwaka
huu watakapoendelea na mahojiano.
Mawakili
hao kwa niaba ya mteja wao wameliomba Jeshi la Polisi kumwandikia barua
rasmi Gwajima, wakiainisha nyaraka wanazozihitaji, pamoja na vifungu
vya sheria vinavyotumiwa na jeshi hilo kutaka nyaraka hizo.
Mawakili
hao wanasema watashukuru kupata hati hiyo ambayo wamedai hawaijui jina,
lakini wanaamini Jeshi la Polisi litafahamu jina la kisheria la nyaraka
husika inayotumika kumtaka Gwajima, awasilishe nyaraka wanazozihitaji.
Aidha wanasema askofu Gwajima atakapopata nyaraka anayoihitaji, atatimiza mwito na kuchukua hatua stahiki za kisheria.
Nyaraka 10
Nyaraka
hizo ni Hati ya Usajili wa Kanisa, Namba ya Usajili, majina ya Baraza
la Wadhamini (Baraza la Kiroho), idadi ya makanisa (matawi)
anayohudumia, nyaraka za helikopta ya Kanisa na muundo wa uongozi wa
Kanisa.
Nyingine
ni Waraka wa Maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na
mali za Kanisa na nyaraka zinazoonesha taarifa za hesabu kutoka kwa
Msajili wa Vyama vya Hiari. Pia waliagizwa kufuatana na mtu anayepiga
picha za video kanisani hapo.
Ushauri
Wakifafanua
kuhusu ubishi huo wa kutaka sheria inayotumiwa na Polisi kuagiza
nyaraka hizo, wanasheria waliozungumza na gazeti hili walisema hakuna
sheria yoyote inayomzuia Polisi kudai umiliki halali wa mali au nyaraka
endapo watazihitaji.
Mwanasheria
Dk Damas Ndumbaro, alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai na
ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, askari Polisi amepewa fursa ya kufanya
ukaguzi wa mali na nyaraka zozote bila ya kuzuiwa na mtu.
‘’Polisi
anaweza kufanya ukaguzi nyumbani kwako bila kuwa na hati ya ukaguzi na
anaweza kuwa nayo. Lengo lao ni kukamilisha masuala yao ya kipolisi
tu,’’ alisema mwanasheria huyo.

No comments:
Post a Comment